Monday, December 28, 2015

Chrsitmass ya marafiki watatu- Mbezi Msakuzi

Mkude, Luanda na Banzi ni marafiki wa siku nyingi. Urafiki wao ulianza baada ya kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza Njombe Sekondari mwaka 1974. Wote watatu wanatoka Matombo Morogoro kama majina yao ynavyosomeka. Hivi sasa wote wanafamilia zao. Kutoka kushoto ni John Banzi na mkewe  Nancy, Lawrence Mkude na mkewe Sango na Bw. Michael Luanda na mkewe Mama Adela. Bw na Bibi Luanda Desemba mwaka huu wametimiza miaka 30 ya ndoa. Pongezi na vigelegele kwa upendo na maisha ya uvumilivu katika ndoa. Hapa tupo nyumbani kwa akina Luanda, Mbezi-Msakuzi jijini Dar (25/12/2015).

No comments: