Friday, January 15, 2016

Sijachelewa-Happy New Year

Kweli sijachelewa. Heri na Baraka za mwaka mpya 2016. Nilishindwa kabisa kuwaaga. Ah, mambo mengi bwana. Mwaka 2015 haukuwa mzuri sana kwangu. Misiba, na kukatika kwa mara kwa mara kwa umeme kumezorotesha mawasiliano yangu kupitia Blog hii, Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2015 niliweza kuning'iniza posts 257 tu ukilinganisha na posts 956 mwaka 2014. Sababu nyingine kubwa ni kuibuka kwa njia nyingine ya mawasiliano hasa Facebook. Mwaka 2015 nimeweza kuweka posts nyingi kupitia facebook za group mbalimbali.Wakati mwingine nimetumia muda mwingi kujishughulisha na Whatsapp. Kilichonipa nguvu kwenye facebook na whatsapp ni kupata feedback kutoka kwa wadau ukilinganisha kwenye blog ambapo ni nadra kupata feedback.

Hata hivyo mwaka 2015 mafanikio haykukosekana kwangu binafsi na kwa familia. Nimeweza kukutana na ndugu na jamaa kupitia vikundi mbalimbali hasa 'Africana Group'   (Pichani). Nimeweza kushiriki shughuli za Kanisa
Kura nilipiga na kushangilia  nyumbani kwangu Kisemvule na kumpata Rais, Mbunge na madiwani.
Nilipata fursa ya kutaniana na uncles kama vile Junior a.k.a 'Davido' pichani
Nawatakia mwaka mpya wa mafanikio na pia tuimarishe mawasiliano kwani maisha ni kuwasiliana.

No comments: