Sunday, November 28, 2010

Dar inaoza!

Jana katika pitapita zangu maeneo ya Kariakoo hasa mtaa wa Msimbazi nilikuta uchafu wa kutisha. Mitaro imeziba na maji machafu yalikuwa ya kitiririka.Ni balaa kabisa. Kama unatembea na viatu vya wazi ni rahisi kabisa kugusa maji hayo machafu na yanukayo.

Tatizo nilionalo ambalo ni kiini cha uchafu uliokithiri jijini ni watu wenyewe. Mitaro imezibwa kwa chupa za maji takataka za mazao mabalimbali na mifuko ya plastiki.

Jambo jingine ni kwamba jiji halina utaratibu mzuri wa kuliweka jiji katika hali ya usafi.Hivi kuna mabwana afya wa jiji kweli. Ah, jamani inabidi kulinda afya za wananchi, aidha jiji lazima livutie kwa usafi. Tujizatiti sote kuiweka DAR ssfi.

No comments: