Sunday, November 28, 2010

Tunaposhindwa kujitosheleza kwa umeme

Ili nchi iweze kuendelea, nishati ya umeme ni lazima ipewe kipaumbele. Nchi nyingi nilizowahi kutembelea hasa Ulaya. Suala la kukosa umeme hata kwa dakika tano tu halijawahi kutokea. Hapa nyumbani ukatikaji wa umeme ni kitu cha kawaida kabisa. Umeme unaweza kukatika hata kwa miezi mitatu na bado kusiwe na uhakika wa kupatikana. Kibaya ni pale ambapo tunapopata maelezo yanayobadilika kila kukicha kutoka kwa mamlaka husika. Leo, Transformer ya Kipawa imeharibika, kesho mtambo wa Songas umeshindwa kuzalisha umeme. Keshokutwa IPTL imekosa mafuta ya kuendesha mitambo, mtondogoo kina cha maji Kidatu kimeshuka. Tatizo ni nini hasa? Kwa kukosa umeme uzalishaji katika sekta zote huathirika. Siyo wakati wa kuweka mkakati. Tunahitaji umeme wa uhakika.

No comments: