Tuesday, August 2, 2011

Na mashine ya kupura mpunga je?

Moja kazi ngumu katika kilimo cha mpunga ni kupura (kutoa punje kwenye mmea). Kwa wakulima wadodo hutumnia njia nyingi iliyo maarufu ni kuupiga kwa kutumia fimbo au kufikicha majani.Unapopiga mpunga uliotandazwa chini mara nyingi ubora wake huathirika sana hasa mchele kuwa na mchanga na harufu ya udongo. Kwa kutumia mashine hii ya Wakorea (pichani) kazi huwa nyepesi na ubora wa mchele huongezeka hivyo kumvutia mlaji.

No comments: