Friday, November 27, 2015

Brass Band kichochezi cha kuanza shule mapema

Nilipokuwa mdogo nilivutiwa sana na Brass Band. Shule ya Msingi Matombo ilkuwa na vifaa vizuri sana vya band kama unavyoviona  kwenye hiyo Brass Band ya Polisi. Ingawa nilikuwa mdogo na mfupi lakini nilitamani kupiga ngoma ndogo,kubwa na pia kuwa Bandmaster  (huyo aliyeshika gongo). Hii ndiyo moja ya sababu iliyonifanya kuanza shule mapema. Na kweli nilipoingia shule nikiwa darasa la nne tu niliweza kuwa mpiga ngoma ndogo, nikiwa darasa la sita ngoma kubwa (huku nikibebewa) na hatimaye Band master (ingawa gongo lilikuwa zito na wakati mwingine kushindwa kuzungusha kwa manjonjo).

No comments: