Saturday, February 18, 2012

Tuanze kufuga bata

Bata ni aina ya ndege wafugwao wanafanana sana na kuku lakini watu wengi hasa Watanzania wanaamini kuwa nyama ya bata imepooza lakini ukijaliwa kutembelea nchi ya Uholanzi mgeni aliyeheshimiwa hukaribishwa nyama ya bata na bei yake ni aghali ukilinganisha na kuku. Ufugaji wa bata ni rahisi ukilinganisha na wa kuku kwani hawashanbuliwi sana na magonjwa na chakula chake hupatikana kirahisi pia wanawezwa kufugwa ndani ya ua au banda.
Ni vizuri sasa watanzania wakahamasika kufuga bata kwani kilishe hana tofauti na kuku. Bei ya bata hapa Dar es Salaam ni kati ya Tshs 15,000-20,000/=

7 comments:

Unknown said...

Naomba nisaidie namba ya mtu ambae anafuga bata. Nataka kununua on a weekly basis. Namba yangu 0718 609944

Unknown said...

ni sahihi kabisa ndugu ttizo watu wamekuwa na iumani potofu kuhusu bata kuwa ni wachafu hivyo huona pian kama nyama yao si nzuri ila ni kukosa elimu sahihi tu bata ni bora kuliko hata kuku hata mayai yake yana protini nzuri zaidi hata kwa watoto na nyama yake ni nzuri sana ila inahitaji ujuzi wa kuipika

Unknown said...

Ni kweli nyama ya bata ni tamu mi nawafuga hao na sasa Nina bats 41 nilianza na bats watatu tu na sasa watatu wanaatamia mayai

mabatamabata said...
This comment has been removed by the author.
pantaleo said...

Bata kwa sasa bei gani wadau?

vedastusy said...

kwa kweli kwa soko la Jiji la Dar es salaam, bei ya bata jogoo kwa sasa limesimama patamu sana ni wastani wa tsh 20000-30000.00 bila ubishi.
ki ukweli ndege huyu akifugwa vizuri anaweza kumtoa mfugaji mapema kuliko kuku wa kienyefi kwani hashambuliwi na maradhi kama alivyo kuku

MAMBO! Inc said...

Nimeanza ufugaji wa bata, nilianza na bata wa5 madume wawili, sasa mmoja ameshaanza kulalia mayai. Ila nataka kujifunza zaidi kuchanganya spishi za mabata (aina tofauti kuwazalisha). Ili wawe wengi na blend tofauti. Kwa anaetaka kunifundisha na masoko napatikana 0715-710002