Friday, January 30, 2015

Benny Morandi kijana anayejituma kuishi maisha bora



Benedict Morandi a.k.a. Bene ni kijana anayeishi kijijini Kiswira, Matombo Morogoro. Kijana huyu ni fundi seremala, mpiga picha, mkulima na mwanakwaya wa Parokia ya Mt. Paulo - Matombo. Ni kijana Mzalendo anayependa kijiji chake. Akiwa mdogo tu Bene tayari alishanunua sehemu yake ya makazi kwa  shilingi 30,000/= tu na hivi sasa amejenga nyumba ya kuishi yeye na familia yake(picha ya juu). Bene anapenda ndugu zake wa upande wa mkewe na wa kwake (picha ya chini). Anaisihi maisha ya kuvutia huku nyumba yake ikizungukwa na madhari mazuri.

No comments: