Monday, April 6, 2009

Hivi ni lazima vilabu vya pombe za kienyeji kuwa hovyo


Vikindu kuna vilabu vingi vya pombe za kienyeji (mnazi, kibuku....). Vilabu vya pombe za kienyeji hutumika zaidi na watu wa kipato cha chini. Licha ya kuwa pombe hizi ni za kienyeji hata hivyo zina wateja wengi hasa kutokana na ukweli kuwa bei yake ni rahisi ukilinganisha na pombe za viwandani.


Blog hii inachotaka kifahamike na wasomaji wake ni hali duni ya vilabu hivi. Mara nyingi utakuta zimeezekwa ovyo ovyo hata vyoo vyake huwa ni vya kubabaisha kabisa. Kunywa pombe ya kienyeji haina maana kuweka mazingira inakopatikana pombe hiyo katika hali dun i. Ni hatari kwa afya zetu. Pichani moja ya klabu cha pombe - Vikindu, Mkuranga.

No comments: