Tuesday, April 7, 2009

Huria iwe na mipaka

Neno huria maana yake ni kufanya utakavyo mradi huvunji sheria. Lakini neno hili likitumiwa vibaya linaweza kuzaa tabia ya kufanya vitu kiholela. Matokeo yake mara nyingi si mazuri. Mara nyingine huzua vifo, mtafaruku na kuathiri kabisa maisha ya jamii. Watu wanauza bidhaa feki ukiuliza utaambiwa hujui bwana soko huria? Watu wanaanzisha dini mbalimbali bila utaratibu- unaambiwa soko huria. Watu wanakojoa barabarani hovyo hovyo -unaambiwa huria. Wenye vyombo vya kusafirisha abiria wanapandisha bei za usafiri wapendavyo kisa soko huria. Huria iwe na mipaka.

No comments: