Monday, April 6, 2009

Kondic alichosema ni kweli

Mara tu baada ya kurejea nyumbani kutoka Cairo, Misri kwenye mechi ya kutafuta Klabu Bingwa Barani Afrika kati ya Yanga na Al-Ahly, Kocha wa Yanga Dusan Kondic alikiri kuwa kiwango cha wapinzani wao kilikuwa ni kikubwa na matarajio ya kushinda mchezo wa marudiano tena kwa magoli mengi ni ndoto.

Kweli tulichoshuhudia Jumamosi ni ukweli wa maneno hayo. Al-Ahly walionyesha kiwango cha hali ya Juu cha soka.

Muda mfupi uliopita nilikutana na rafiki yangu Msuya shabiki wa Yanga pale "Kempiski" leo hakuwa na maneno mengi alisema kuwa alitamani kuendelea soka lile japokuwa walikuwa wamefungwa. Kumbe alichosema Kondic ni kweli. Wakati mwingine tuwe wa kweli tu kama Kondic.

2 comments:

Belo said...

Mimi ni mshabiki wa Yanga lakini huyo Kondic hatufai na alichemsha kupanga list kule Misri alitakiwa kupanga kikosi cha defence then tukija huku ndio apange 4-4-2

Innocent John Banzi said...

Belo, pole sana.
Tunachojua sisi watoto wa Msimbazi. Yanga haina ubavu wa kukabiliana na waarabu. Historia tunayo sisi waulize Zamalek walipovuliwa ubingwa nyumbani kwao. Nasi tulifanya mapokezi makubwa kwa vijana wetu. Hata kama Kondic angepanga timu yenye kujihami zaidi wakati mlipokuwa Cairo msingewaweza akina Aboutrika!