Tuesday, April 7, 2009

Sasa wananchi wameamka

Ni leo hii mchana wakati nilipofika kituoni Kisemvule kupanda bus la kwenda Mbagala nilikuta bango lililoandikwa- Kisemvule Mbagala - sh 400/- huku wazee kwa vijana pamoja na viongozi wa kijiji wakisimamia tangazo hili na kutuelekeza wananchi tunaosafiri kuwa tusiwe tayari kulipa zaidi ya shilingi 400/-.

Jana nililipa shilingi 600/-. Leo mambo yamebadilika kabisa. Wananchi wamechachamaa, wanaona wanadhulumiwa kabisa. Bei zilitangazwa kushushwa lakini wenye magari hawakutaka kushusha. Ssaa wananchi wameamka na nguvu yao ni kubwa. Umoja ni nguvu.

No comments: