Monday, April 20, 2009

Kwa mara ya kwanza nauli njia ya Mkuranga imeshuka!

Kwa abiria wanaosafiri kwa magari madogo yaendeayo njia ya Mkuranga kutoka Mbagala Rangi 3 nauli imepungua kwa asilimia 36. Kwa mfano Mbagala Vikindu sasa shilingi 300 badala ya shilingi 500 na Mbagala-Kisemvule sasa shilingi 400 bei ya zamani shilingi 600. Hii ni kwa mara ya kwanza kwa gharama za usafiri kushuka kwa njia hiyo. Mara kwa mara abiria wengi ambao ni wakulima wamekuwa wakipata wakati mgumu kwa kutozwa nauli za juu kutoka Mbagala kwenda Mwandege, Vikindu, Kisemvule na Mkuranga.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya wanavijiji wa sehemu hizo kupatiwa jedwali kutoka SUMATRA inayoelezea viwango vya nauli na kusimamia kwa ukamilifu utekelezaji wake.

No comments: