Wednesday, August 26, 2009

Poleni wa Idodi-Hatuna budi kujifunza


Napata picha isiyo furahisha, picha ya majonzi. Vifo. Kwa ajali ya moto. Tena wanafunzi, zaidi ya hapo ni wasichana. Wamefariki wakitafuta elimu ndo kwanza wameanza safari. Tegemeo la taifa. Tumepoteza vijana 12. Msiba mkubwa. Poleni wa Idodi.

Labda ni vizuri nikasema kuwa inatubidi kuwa makini zaidi katika masuala haya ya Jumuiya. Wanapokuwa watu wengi kuna la ziada. Kwa wanafunzi kuna zaidi ya ziada. Wanafunzi wanaweza kufanya lolote katika mazingira yoyote pengine bila kutambua madhara yake. Wanaweza kugoma wakaharibu vifaa, wakawapiga walimu na wanafunzi wenzao kwa lengo la kutekelezewa wanachotaka sasa hivi.

Huyu aliyewasha mshumaa ili ajisomee hakuwa na lengo baya. Yeye alifikiri kufaulu mitihani. Suala la mshumaa kuweza kusababisha moto huenda halikuwepo. Ni wajibu kwa viongozi kutambua hayo na ndipo kazi ya ulinzi inapokuwa ni umuhimu.

Ulinzi ni usalama wa watu na mali zao. Wangekuwepo walinzi makini wangeweza kupita kwenye bweni hilo mapema na kubaini kuwa kuna mshumaa uliowashwa bila kuzimwa baada ya muda kupita na kama doria ingefanywa kila kipindi kifupi hili huenda lingegundulika mapema. Kweli ni bahati mbaya lakini hatuna bundi kujifunza lisitokee tena. Ni uchungu mkubwa kwa kweli kupoteza vijana 12 kwa muda mfupi.

1 comment:

Belo said...

Kuna umuhimu wa kila shuele ya bweni iwe na Fire Extinguisher na wanafunzi na walimu wafundishwe kuzitumia.Ukweli wanafunzi wengi hutumia mshumaa kusomea hasa mitihani ikikaribia