Tuesday, January 4, 2011

Katiba Mpya sawa uelewa je?

Ni kweli kuna haja ya kuwa na Katiba Mpya kwa mazingira ya sasa. Lakini wanaoipigia debe si wananchi wa kawaida. "Wajanja wanatafuta ajira hasa wasomi kwa gharama ya walalahoi." Nilimsikia jamaa mmoja akinena nikiwa ndani ya Daladala juzi Jumapili.

2 comments:

Belo said...

Mimi nafikiri kwanza hiyo katiba iliyopo wananchi wengi hawaifahamu,kwa hiyo serikali iweke mkakati(mashuleni na kwenye jamii) ili wananchi wote waifahamu halafu ndio waangalie kama kuna umuhimu wa kuibadili.Kwa sasa sidhani hata 5% ya Watanzania kama wanaifhamu katiba

Banzi wa Moro said...

Ndiyo Bw.Belo ni kweli ni asilimia ndogo sana ya watanzania wanaoifahamu Katiba iliyoandikwa. Lakini Katiba si kitabu ni utaratibu uliowekwa ili kuiongoza jamii mahali fulani kutekeleza majukumu yao. Kuna baadhi ya nchi tena zilizoendelea hazina Katiba iliyoandikwa lakini wanatekeleza majukumu yao bila matatizo. Lakini hapa kwetu ni kweli kuna umuhimu wa KATIBA kufanyiwa mabadiliko kwani muda umeshapita na mazingira yamebadilika kwa kiasi kikubwa. Vyama vingi vya kisiasa na mambo mengine.