Wednesday, April 22, 2015

Enzi za usafiri wa mabus ya EAR (RAB)

Kwa mara ya kwanza nilisafiri kwa bus la EAR kwenda Njombe masomoni kidato cha kwanza Njombe Secondary School mwaka 1974. Safari yangu ilianzia Morogoro Railway Station. Mabus haya yalikuwa na utaratibu mzuri. Yalikuwa na madaraja mawili  la kwanza na la pili (mimi nilisafiri daraja la pili tena kwa kutmia 'Government warrant'). Madereva wake walikuwa ni watu wazima. Hawakuwa wakienda kwa mwendo kasi, kulikuwa na vituo maalum vya kuyakagua mabus hayo na kuyafanyia service pamoja na kuweka mafuta. Kituo kimojawapo ni Mikumi kabla hujaanza kuupanda mlima Kitonga ukitokea Morogoro. Ukifika Iringa  ilikuwepo station kubwa ya mabus ya railways. Hapa mabus hukaguliwa na abiria wanaoendelea na safari hupumzika kwa muda mrefu kabla ya kupatiwa bus lingine kwa safari. Barabara hazikuwa nzuri sana. Ninamshukuru Mungu kwa kipindi chote cha miaka sita nilioishi kama mwanafunzi mkoani Iringa nikisafiri kwa mabus ya 'RAB' ajali zilikuwa chache sana na wala sikumbuki kama iliwahi kutokea. Hivi sasa barabara zimeboreshwa, magari ni ya kisasa zaidi na kila mmoja wetu anaweza kuendesha magari ya abiria (buses). Kila kukicha ni ajali mbaya tena zenye kuua abiria. Hivi hatuwezi angalau kupunguza ajali hizi?

No comments: