Thursday, April 30, 2015

Nakukumbuka Mjomba Balozi Daniel Mloka

Hii ni picha ya kaburi alilozikwa Balozi Daniel Narcis Mtonga Mloka. Haya ni makaburi ya Parokia ya Mt.Paulo ya Matombo. Ndugu zangu wengi wamezikwa hapa akiwemo mama yangu mzazi.Ni miaka zaidi ya 21 sasa tangu Balozi Mloka atuache ghafla wakati ambapo wengi tulikuwa tunamtegemea. Kitu kimoja ambacho Balozi Mloka alinifundisha ni kuandika na kweli alikuwa ni mwandishi mzuri ingawa fani yake halisi ni uchumi. Nakumbuka nikiwa likizo nyumbani kwake Stockholm - Sweden wakati huo mimi nasoma Soviet Union au Urusi, tuliweza kuandika kitabu (Nitawaeleza siku nyingi title ya kitabu hicho nadhani hatkufanikiwa kukitoa).Balozi Mloka alikuwa anatambua azungumze nini na mbele ya nani. Pamoja ya kwamba alikuwa uncle wangu, mumewe shangazi yangu dada wa baba yangu. Balozi Mloka alikuwa ni rafiki yangu wa kweli. Pumzika uncle Balozi Mloka.

No comments: