Wednesday, June 30, 2010

Hili lipo pia Dar


Nilishangaa kuona picha hii katika gazeti la mwananchi la tarehe 26/6/2010. Hii ni nyumba ya mkazi mmoja wa jijini anaitwa Yose Francis. Amekuwa akiishi katika mazingira haya kwa muda wa miaka 10 sasa. Makazi haya yako katika wilaya ya Temeke. Hebu jiulize huduma ya choo anaipata wapi mkazi huyu? Mamlaka zinazohusika zimelifumbia macho hili kwa muda wa miaka 10? Hii ni hatari.

No comments: