Thursday, June 24, 2010

Mwezi wa sita nilitingwa


Kama kuna mwezi ambao nimetingwa sana hadi sasa ni mwezi wa sita. Wasomaji wangu wa Banzi wa Moro hawajanisoma tangu mwezi uanze na sasa unakaribia kufikia ukingoni.

Kwa wasiofahamu huu ni mwisho wa mwaka wa serikali shughuli ni nyingi kweli kwa wafanyakazi wa serikali na ni kipindi hiki ambacho bajeti ya serikali husomwa kwa ajili ya mwaka ujao wa fedha. Mwezi huu wa sita nimeweza kusafiri kikazi kwenda mikoa ya Pwani (hususani Wilaya ya Mkuranga na Kibaha), Mkoa wa Tanga (Muheza na Pangani) kwa shughuli za kupelemba na kutathmini shughuli za utafiti wa kilimo hapa nchini.

Jana nimerudi kutoka Dodoma ambako nilihudhuria kikao cha Bunge ambacho Wizara ninayofanyia kazi iliwasilisha Bajeti yake na kupita siku hiyo hiyo bila mizengwe!

Kote nilikopita nimeona mengi na kujifunza mengi. Muda ukiruhusu nitawarushia baadhi ya yale niliyoyaona nikiwa huko.

No comments: