Wednesday, June 30, 2010

Watafiti wa Mikocheni waanza kutafiti maembe


Watafiti wa kituo cha Utafiti Mikocheni kilichopo jijini Dar, wameanza kufanya utafiti wa uzalishaji wa maembe. Utafiti wao unalenga katika kupambana na nzi wa matunda (fruit fly) ambaye husababisha maembe kuoza na kupunguza ubora wa maembe na hatimaye kukosa soko ndani na nje ya nchi. Utafiti mwingine ni ule wa kutafuta aina bora za maembe kwa mahitaji mbalimbali. Tayari miche imeanza kuoteshwa katika kituo kidogo cha utafiti Mkuranga.

No comments: