Monday, June 28, 2010

Ng'ombe wa mfugaji Lugoba


Kijiji cha Lugoba mkoa wa Pwani ni cha wakulima na wafugaji. Katika shughuli za kupelemba na kutathmini shughuli za utafiti. Tulimtembelea mfugaji mmoja na kutueleza mengi kuhusu ufugaji mafanikio na changamoto anazozipata. Pichani ni baadhi ya ng'ombe wa mfugaji huyu ambaye kwa maneno yake mwenyewe amesema kuwa ng'ombe bora mwenye umri wa miaka mitatu aliyetunzwa vizuri anaweza kuwa na uzito wa kilo 500-600 ambaye anaweza kuuzwa sokoni kwa bei ya shilingi 1,000,000 hadi 1,500,000. We acha tu ufugaji unalipa.

No comments: