Monday, March 12, 2012

Masomoni Swaziland

Nimewasili nchini Swaziland jana tarehe 11/03/2012 kwa madhumuni ya mafunzo ya muda mfupi. Nipo chuoni Mananga kilichopo mji mdogo ujulikanao Ezuilini. Swaziland ni nchi ya vilima vilima.Nimefahamishwa kuwa idadi ya watu nchi nzima ni watu milioni 1.2 ni watu wachache sana karibu hii ni robo ya idadi ya watu walioko jijini Dar Es Salaam.Uchumi wa nchi hii hutegemea kilimo cha miwa. Swaziland inaoongozwa na King Mswati. Pasaka tutakula wote hapo nyumbani. Mkiona kimya nimetingwa na shule!1600

3 comments:

sophia said...

Nakutakia kila la kheri ndugu yangu, nami natarajia kuwa nyumbani kipindi cha pasaka

sophia said...

Nakutakia kila la kheri ndugu yangu, nami natarajia kuwa nyumbani kipindi cha pasaka

Banzi wa Moro said...

Asante mama Lulu.Natumaini tutaonana nyumbani na karibu kwa Pasaka. Huku kitabu kizuri tu hata ukiwa peke yako unafundishwa ni tailor made course anaeleza mahitaji yako wanakupa dose sawasawa labda ujifanye unajua!