Sunday, March 25, 2012

Nimesali Kanisa la Mt.Dolorosa-Mbabane,Swaziland

Leo Jumapili nimebahatika kusali katika Kanisa Katoliki la Mt. Dolorosa lililoko jijini Mbabane-Swaziland.Ni bahati iliyoje kusali kwenye Kanisa ambalo jina lake ni jina la mama mdogo Dolorasa wa Makuburi, Dar.

Kanisa hili ni kubwa kiasi na limejengwa kwa muundo wa msalaba.Ibada niliyohudhuria iliendeshwa kwa lugha ya Kiingereza. Ibada katika kanisa hili huendesha kwa lugha kuu tatu-Kiswati,Kiingereza na Kireno. Kwa kawaida misa ya pili saa 2.00 ni ya Kiingereza na saa 4.30 ni Kiswati kila Jumapili. Lakini Jumapili ya kwanza na ya tatu ya mwezi misa ya pili huwa ni ya Kireno.
Nilichoona.
Taratibu zote za ibada ni sawa kabisa kama tunavyoendesha ibada zetu(katoliki)Tanzania. Tatizo ni lile lile vijana wanaohudhuria ibada ni wachache. Utoaji wa sadaka bado ni mdogo na sarafu hotelwa pia!Ingawa hawatangazi kilichopatikana. (huenda wanaweka kwenye mbao za matangazo). Sikuona vipaji hapa (nafikiri sisi tunafanya vizuri).Wachelewaji wapo, na hata baada ya mahubiri hurusihusiwa kuingia.

Hata hivyo nimefurahishwa na utaratbu wanaoutumia wa kutenga sehemu za mbele kwa ajili ya watoto wadogo.Mabechi yao ni kama ya wakubwa tu. Nao huingia kanisani baada ya kutoa sadaka, nafikiri kabla ya hapo huwa na Sunday school (sina uhakika)halafu hupewa fursa ya kuimba angalau wimbo mmoja (waliimba kwa Kiswati).Pia hakuna matangazo yasiyo ya lazima na misa inaanza kwa wakati uliopangwa. Nilipomuuliza Chris Sibandze (siyo mkatoliki) kwanini vijana hawaendi kanisani alinijibu pengine wanavutiwa zaidi na makanisa yaliyoibuka siku hizi ambayo huendesha ibada hata kwenye viwanja vya mpira na hakuna anayejali na kinachoendelea!Nakushukuru sana Bw. Chris kwa kunipeleka kanisani.Katikati ya jiji hili la Mbabane ndipo lilipo Kanisa Katoliki Mt.Dolorosa.

No comments: