Tuesday, May 26, 2009

Wakulima wa alizeti waanza kuzalisha mbegu bora

Wilaya ya Iramba inatarajia kuboresha uzalishaji wa alizeti kutokana na mpango waliouanzisha kwa baadhi ya wakulima kuanza kuzalisha mbegu bora za alizeti.Hali hiyp imebainika baada ya watafiti wa kilimo na mifugo kutoka makao makuu ya Wizara ya Kilimo na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Mifugo kutembelea wilaya hiyo hivi karibuni kwa lengo la kupelemba na kutathmini shughuli za utafiti kanda ya kati.

Mbegu bora ya alizeti inayozalishwa inatarajiwa kuuzwa kati ya shilingi 2000 na 2500 kwa kilo na kupatikana kwa urahisi kwa wakulima huko vijijini. Aina ya mbegu ya alizeti inayozalishwa ni Record.

Si rahisi kwa mfugaji kutoa idadi ya mifugo yake

Ni masaa machache tangu niondoke kijiji cha Kaselya wilayani Iramba. Timu yetu ya Kupelemba na kutathmini ilifika hapa kuona jinsi ng'ombe aina ya Mpwapwa walionunuliwa na baadhi ya wafugaji katika kijiji hicho mwaka 2005 wanavyofugwa na kunufaisha wafugaji. Ng'ombe wanaendelea vizuri na lengo la kuboresha ng'ombe wa asili kwa kupitia madume ya Mpwapwa linaonyesha kufanikiwa. Jambo ambalo sikulitegemea ni kwa mfugaji mmoja kukataa kutoa idadi ya ng'ombe alionao.

Iramba ni alizeti

Leo nilisafiri kwenda wilaya ya Iramba kuona shughuli za kilimo zinavyoendeshwa na wakulima wa wilaya hiyo na hususan jinsi watafiti na wagani wanavyopeleka teknolojia kwa wakulima.

Lazima nikiri kwamba hii ni mara yangu ya kwanza kufika Iramba. Nikiwa njiani nilivutiwa na mashamba ya alizeti yaliyolimwa kando kando ya barabara ya kwenda Mwanza. Mashamba ni ya ukubwa wa wastani.Licha ya ukame ulioikumba kanda ya kati alizeti imekubali. Msafara wetu ulipata kufanya mazungumza na afisa wa kilimo wa wilaya na kueleza kuwa hali inavyoonekana uzalishaji mwaka huu utaongezeka ukilinganisha na mwaka wa jana na kwa hali hiyo kuna hatari ya kuwa na tatizo la soko la alizeti. Kwasasa gunia linauzwa kwa bei ya Tshs 15,000 wakati msimu wa mwaka jana gunia moja liliuzwa kwa bei ya Tshs 30,0000. Kweli Iramba ni alizeti.

Sunday, May 24, 2009

CETAWICO KUTATUA SOKO LA ZABIBU


Kiwanda cha mvinyo cha CETAWICO kilichopo Dodoma (Hombolo) kimedhamiria kuondoa tatizo la soko la zabibu kwa wakulima wa zao hilo. Hayo yalisemwa na Mhandisi Njovu alipoongea na Banzi wa Moro hivi karibuni alipotembelea kiwanda hicho katika shughuli za kupelemba na kutathmi shughuli za utafiti kanda ya kati. Uhakika huo unatokana na kiwanda hicho kupanua uwezo wa kuzalisha mvinyo kwa kuboresha mitambo na vifaa vingine. CETAWICO kwa sasa inazlisha aina kadhaa za mvinyo zikiwemo zile za Presidential na The Last Super.Bei ya zabibu kwa sasa ni kati ya Tshs 500-800 kwa kilo. Kwa muda mrefu wakulima wa zabibu wamekuwa wakilalamikia soko la zao hilo na kusababisha uzalishaji wa zabibu kushuka hapa nchini.

Kichwa kikubwa cha alizeti

Nilipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Hombolo hivi karibuni nilivutiwa na mimea ya alizeti yenye vichwa vikubwa nikidhani kuwa kichwa kikubwa ni ubora wa alizeti lakini kumbe sivyo, watafiti walinieleza kuwa ili kuwa na mbegu nyingi za alizeti zilizojaa vizuri mmea unatakiwa kuwa na kichwa cha wastani. Ukitaka kufahamu zaidi kuhusu hilo wasiliana na watafiti wa mazao wa kituo cha Hombolo au kwenye vituo vya utafiti wa mazao vilivyopo karibu nawe. Kweli pua kubwa si wingi wa makamasi!

Hombolo waendelea na utafiti wa mtama

Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Hombolo iliyopo mkoani Dodoma kanda ya kati iko mbioni kutoa aina mpya za mtama zinazoweza kuhimili ukame na kuzaa kwa wingi pamoja na kutoa aina ya mtama itakayoweza kutumika kwa kutengeneza nishati (mafuta). Akiongea na blog hii hivi karibuni, Mtafiti Mkuu Bw. Letayo alisema kuwa tafiti hizi zinafanyika kwa ushirikiano na Asasi ya Utafiti ya Kimataifa ijulikanayo ICRISAT. Utafiti unaendelea vizuri na matokeo ya awali yanaonyesha mafanikio.

Mbuzi wa asili 'gogo white" kuboreshwa


Watafiti wa mifugo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Nchini (NLRI) wameanza utafiti wa kuboresha mbuzi wa asili wajulikanao kwa jina la "gogo white" ili waweze kupata aina mpya ya mbuzi atakayeweza kuwa na sifa za kutoa nyama nyingi na nzuri pamoja na maziwa ya kutosha na pia kuhimili magonjwa na wadudu. Kazi hii ya utafiti tayari imeshaanza katika vituo cha Utafiti wa Mifugo Mpwapwa na Kituo cha Utafiti wa Malisho cha Kongwa vilivyopo Dodoma. Iwapo watafanikiwa basi wataweza kutoa jawabu kwa wafugaji wa mbuzi wanaopenda kufuga mbuzi aina ya "gogo white." Blog hii ilipata kuwaona mbuzi hao hivi karibuni wakiwa katika sehemu zao za utafiti. Mbuzi hao wanavutia kwa rangi zao nyeupe na maumbo yao.

Tatizo la usafiri mikoa ya kati na ziwa sasa kuwa historia

Leo hii mchana nimewasili Singida mjini nikitokea Dodoma kikazi. Kilichonifurahisha ni kuona kuwa sehemu kubwa ya matengenezo ya barabara imekamilika. Mlima mbaya wa Saranda uliokuwa unawatesa madereva umeshatiwa lami. Ni sehemu ndogo kabisa ambayo bado haijakamilika. Njiani tulikutana na mabus kutoka Mwanza na Tabora yakifukia na ni mengi. Ndo maana nasema kuwa barabara hiyo itakapokamilika usafiri kwa mikoa ya kati na ziwa utaboreshwa kwa kiwango kikubwa na utakuwa ni wa uhakika zaidi.

Thursday, May 14, 2009

Bunge la Bajeti laja

Kikao kinachofuata cha Bunge ni Bunge la Bajeti. Ni Bunge linalotoa ruhusu ya kutekeleza mipango ya wizara mbalimbali inayotarajia kuifanya kwa mwaka 2009/10. Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2008/09 utatolewa pia katika kikao hicho cha Bunge. Wabunge watajadili na kupitisha Bajeti kwa utekelezaji. Lakini ni vizuri tujiulize ni kweli tunatekeleza kilichopo kwenye Bajeti? Je, fedha zinatolewa kama ilivyopitishwa na Bunge? Hili bado nashindwa kuelewa.

Nani kasema bora vita

Mabomu yaliyolipuka na yanayoendelea kulipuka maeneo ya Mbagala jijini Dar es Salaam ni kiashiria tosha kuwa vita si lele mama. Ukiwa umeshiba unafanya shughuli zako tatizo dogo tu unasema heri tupigane tu! Ah bwana wee umeshaiona vita wewe. Athari za vita ni nyingi sana. Mabomu ya Mbagala iwe fundisho.

Barcelona Vs Manchester United ni fainali ya kweli

Kiwango walichonacho sasa timu hizi mbili kinatoa burudani kwa wapenzi wa kandanda.
Unapoingalia Barcelona wakicheza unaona team work unaona kila mchezaji ni kifaa. Hebu mwangalie Mesi, tupa jicho kwa Etoo na jaribu kumfuatilia Iniesta ni tishio kweli. Hivyo hivyo kwa Manchester kuna Ronaldo, Rooney, Rio Ferdinand na wengineo kwa vyovyote vile wameonyesha uwezo mkubwa kwa msimu huu ndiyo maana nasema, Barca Vs Man U ni fainali ya kweli.

Mungukiki wanasumbua Kenya

Kenya si salama. Wananchi wanasumbuliwa na kikundi cha mauaji cha Mungukiki. Kinavamia na kuua wakati mwingine kijiji kuteketezwa kwa moto. Hawa ndiyo Mungukiki. Tuombe Mungu kusiwe na kikundi kama hiki hapa Tanzania. Ni balaa.

Mkwawa wa Yanga


Hufurahi Yanga inaposhinda kama anavyoonekana kwenye picha.
Huchukia Yanga inapofanya vibaya.
Ana maneno mengi ya unazi na wakati mwingine ya mauzi
Angalia hata picha hii ameipiga kwenye maua ya njano na kijani (Rangi ya Yanga)

Lukuvi tawire tunataka kuiona Bandarisalama iliyo safi

Tunataka viongozi wanaokuja na vision yao. Lukuvi ameliona jiji la Dar Es Salaam ni chafu kwa hiyo amewataka viongozi na wakazi wa jiji la Dar Es Salaam kuliweka jiji hilo katika hali ya usafi ili lipendeze liwe jiji kweli. Banzi wa Moro anaona kuwa kikubwa ni kusimamia utekelezaji wake. Watu wanatupa takataka ovyo na kuchafua jiji tunawaona na tunawaacha, watu wakojoa ovyo mitaani tunaowaon na kuwaacha hivi hivi. Tutakukumbuka Lukuvi tutakukumbuka kama utaliweka jiji la Dar katika hali ya usafi nafikiri itakuwa ni output yako moja nzuri.

Unapochelewa "flight"

Usafiri wa ndege ni tofauti kabisa na usafiri wa bus. Kabla ndege haijapaa. Abiria hupitia mchakato unaochukua muda mrefu. Ndiyo maana unaambiwa ufike kiwanjani saa 2.00 au moja kabla ya safari kuanza. Kwani kuna ukaguzi wa ticket, pasi mizigo na usalama wa abiria. Unapofika kiwanjani dakika 45 kabla ya safari kuanza mara nyingi unahesabiwa kuwa umechelewa na kwa kweli ndege haiwezi kukusubiri. Usafiri wa bus ni tofauti kabisa hata ukichelewa unaweza ukakodi taxi ukalikimbiza bus na kupandia Kibaha! Lakini ndege utaikatizia wapi! Banzi wa Moro anawatahadharisha wanaosafiri kwa ndege kufika uwanjani mapema kupeleka usumbufu usio wa lazima unaoweza kusababisha kukosa safari au kubadilisha flight kwa kulipia gharama nyingine hivyo kufanya kuchelewa unakotakiwa kwenda na kuharibu mipango yote hasa unapokwenda kwa safari ya kikazi.