Thursday, August 19, 2010

Choroko zawapatia wakulima wa Nanyumbu bilioni 1.5



Habari iliyoandikwa kwenye gazeti la Mwananchi la tarehe 19 Agosti 2010 ukurasa wa 5 kuhusu choroko zinasisimua na kuhamasisha kulima. Hebu fikiria zao la choroko lilivyoweza kuwaingizia wakulima wa wilaya ya Nanyumbu kipato cha shilingi bilioni 1.5 msimu uliopita. Kwa kweli hiki ni kiasi kingi cha fedha. Kwa mazoea, wakulima wa Nanyumbu hutegemea Korosho kama zao la biashara. Msimu uliopita kilo ya choroko ilinunuliwa kwa shilingi 1,500 wakati korosho zilinunuliwa kwa shilingi 994 kwa kilo. Hii inatupa picha kuwa si lazima ulime mahindi au mpunga ili uweze kupata kipato na kuboresha maisha yako, choroko nazo zinalipa tena sana!

No comments: