Monday, January 30, 2012

Matombo Msalabani

Hii ni moja ya alama kuu ya Tarafa ya Matombo-Matombo msalabani. Ukifika Msalabani ni rahisi kwenda Mtamba (Makao makuu ya tarafa ya Matombo), Matombo Mission/Matombo Secondary School, vijiji vya Kibungo, Tawa, Lukenge, Dimilo, Konde, Kitungwa, Lusangalala, Mlono n.k. (hiyo barabara inayoonekana pichani). Picha hii ni zawadi kutoka kwa Bw. Gaitan Banzi aliyekuwa huko nyumbani Matombo kwa likizo. Nami nasema asante kwa zawadi nzuri. Wengi wetu hufikiri zawadi zinazoshikika kama vile maembe, ndizi, kuku, mchele,mashelisheli, mafenesi n.k.Kumbukumbu kama hii ni zawadi ya kudumu . Embe, kuku, 'ubwabwa' utakula utasahau! Tulipokuwa wadogo mimi na kaka yangu marehemu George Banzi tulikuwa tunajiuliza maswali mengi kuhusu msalaba huu. Kaka George alikwenda mbali zaidi akifikiri kuwa huenda Wajerumani wameficha fedha humo ndani! Nangojea zawadi nyingine kutoka Matombo pamoja na ile ya picha ya jiwe la Matombo!

7 comments:

Gaitan John said...

Nimefarijika sana kuona shemeji umeweka picha hii kwenye blog yako. Lilitujia wazo la kupiga picha msalaba huu wakati tukisubiri gari pale. Ningekuomba shemeji ungetoa historia ya msalaba huu kujengwa kwani mimi nafahamu kidogo zaidi yako hivyo watu watakosa historia kamili. Nakuomba sana kwa hilo kwani watu wengi hawafahamu kwanini umejengwa pale

Innocent John Banzi said...

Gaitan naomba uniandikie kwa hilo unalofahamu kuhusu historia ya msalaba huo nami nitaipost kwenye Banzi wa Moro ili watu waisome na kuwa kumbukumbu ya vizazi vijavyo.

john said...

dah nimepapenda mimi nimefika tawa ila nimepapenda sana

mkazuzu said...

nyumban kwetu pazuri sana