Tuesday, August 26, 2014

Hivi Tanzania tumeshindwa kumuungamiza mbu!

Ni mdudu mdogo sana. Lakini anaonekana kwa macho. Bakteria  haonekani kwa macho,kirusi haonekani kwa macho lakini nguvu nyingi zinatumika kupambana nao. Huyu mdudu mbu anayeonekana kwa macho kwanini tumeshindwa kumuungamiza wakati anatuletea maafa makubwa? Si wengi ambao wanaogua ukimwi hapa nchini. Lakini ni nani asiyegua Malaria? Vifo vingi hapa nchini vinasababishwa na Malaria hasa vya watoto. Hivi kweli tumeshindwa kuwaangamiza mbu kwa kuboresha usafi? Tumeshindwa kuwaangamiza mbu kwa kuwaua na madawa? Vyandarua sawa, lakini ni nani anyetumia ipasavyo?Ni wangapi wenye uwezo wa kununua vyandarua?

Tukae chini tuanze upya na tuanze sasa kuangamiza mbu kwa nguvu zote, tutafanikiwa. Tusisubiri misaada ya kutoka nje inasaidia lakini haitotokomeza adui mbu. Hebu tujiulize hivi kweli kama mbu angekuwa tishio ulaya wangekaa kimya? Hata, Nguvu zote zingeelekezwa huko. Hili linaniumiza na imebidi niliandike.

No comments: