Tuesday, May 6, 2014

Matombo-msimu wa machungwa na machenza

Huu ni msimu wa machungwa na machenza kijijini Matombo, Morogoro. Hata hivyo Banzi wa Moro alipokuwa kijijini hapo hivi karibuni hakufurahishwa na jinsi biashara ya matunda hayo inavyofanyika kwa sasa. Walanguzi hununua matunda hayo yangali machanga na kuyavuna hivyo kushusha ubora wake. Walaji wengi wamekuwa wakilalamikia ladha ya matunda hayo yanayotoka Matombo.. Matombo imepoteza sifa ya kuwa na machungwa makubwa na matamu. Wakulima na wananchi wa Matombo wakisaidiwa na Viongozi wao hawanabudi kulitatua tatizo hili ili wakulima waweze kuuza matunda yaliyo bora yanayopendwa na walaji hivyo kujipatia kipato cha kutosha  kwa kuuza kwa bei yenye faida kubwa. Nimefahamishwa kuwa bei ya jumla ya chungwa moja au chenza ni shilingi kumi.

No comments: