Wednesday, March 4, 2009

Tusipokuwa makini hata ziwa Victoria litapotea

Tusifikiri utani tunapoambiwa kuwa tusikate miti. Tutunze mazingira.Watu wengine wanafikiri ni masihara. Tusipokuwa makini hata ziwa Victoria linaweza kupotea!

Leo mchana Mkurugenzi Mtendaji wa ASARECA Dr.S.Ketema aliwasilisha mada ambayo ilivutia sana wakati mwingine iliniweka katika fikra nzito na tafakari ya kina yenye kukata tamaa lakini wakati mwingine kuwa na matumaini iwapo tutapambana haraka kunusuru hali ya sasa. Hii yote inatokana na hali halisi ilivyo katika ulimwengu huu tunaoishi.

Moja ya mfano hai alioutoa ni ziwa lilikuwepo Ethiopia miaka 20 iliyopita sasa limekauka kabisa kiasi cha kufanya watu waanze kulima kwenye eneo lote lililokuwemo ziwa. Hii yote ni kutokana na kutokuwa makini katika utunzaji wa mazingira.Watu wamekata miti ovyo kwa muda mrefu na hivyo kuathiri mazingira yanayolizunguka ziwa hilo.Tatizo si kukauka kwa ziwa tu bali ni jinsi uzalishaji unavyoathirika na hatimaye kuathiri maisha ya watu.

No comments: