Monday, December 2, 2013

Nimempoteza mdogo wangu Emmanuel Kishongo

Emmanuel Kishongo alifariki ghafla siku ya 24/11/2013- Jumapili huko Chalinze mkoa wa Pwani akiwa na umri wa takribani miaka 41. Emmanuel ni mdogo wangu mtoto wa mama mdogo. Amezaliwa wakati niko darasa la sita hivyo namfahamu sana. Alikuwa ni kIchwa darasani na pia katika maisha. Mpambanaji na mfanya biashara aliyekuwa anachipukia kwa kasi.

Mara baada ya kuhitimu kidato cha sita alijiunga na  Chuo cha Mzumbe wakati huo kikiitwa IDM-Mzumbe kwa masomo ya Diploma ya Juu ya Uchumi na Mipango. Baada ya kuhitimu aliamua kujiajiri mwenyewe  hadi umauti ulipomkuta.

Emma umeniliza kwa kuwa daima ulikuwa mstari wa mbele kutuunganisha wanandugu. Nakumbuka kuna siku uliniambia kuwa "Kaka tutafutane, tupeana taarifa kwa jambo lolote na tusaidiane pale inapowezekana." Kweli, Emma baada ya hapo ulikuwa daima ukitekeleza usemi wako hadi kufa kwako. Emma ulikuwa moja ya majembe ya familia. Tumekupoteza  wakati ambapo ndiyo umeanza kuweka msingi imara wa ushirikiano. Nakumbuka jinsi ulivyoendesha gari lako kutoka Mzumbe hadi Dar wakati marehemu mjomba wetu Dr. Gregory Mluge alipolazwa hosptalini Mhumbili. Bado nakumbuka jinsi ulivyokuja na familia yako kwenye sherehe ya dada yetu Anna Mdimi huku ukiwa umelowa jasho mwili mzima, alipokuja kwenye sherehe ya kounio ya mwanao Eka Kamsopi Mdimi na pale kupiga picha ya pamoja. Nakumbuka pia jinsi ulivyochangia matibabu ya mdogo wetu  Dikupatile Wilbart mara ulipopata taarifa. Hakika baada ya kupata taarifa ya kifo chako nililia kwa uchungu. Na nitaendelea kulia kila nitakapokukumbuka. Nina matumaini siku moja tutakutana huko ulikokwenda wewe! Ninakuombea daima. AMINA. Emmanuel Kishongo amezikwa tarehe 27/11/2013 nyumbani kwake Mzumbe-Changarawe-MOROGORO

No comments: