Wednesday, December 11, 2013

Marafiki tuwapende na watoto wetu pia

Tulipopata nafasi ya kutembelea familia ya Baba Herieth wa Kisemvule tulifurahi na watoto wake pia. Ilikuwa ni usiku. Lakini watoto walifurahi. Baba Herieth alinitoa nyumbani kwangu wakati nikiangali bustani yangu na kuniambia twende nyumbani kwake tukiwa na rafiki yetu Marara. Mama Herieth alishtukia ugeni umeingia. Walipotusindikiza tukapewa zawadi ya miwa na mananasi mpingo. Huo ndiyo Uafrika wenyewe hakuna mwaliko rasmi. Furaha ya mwenyeji ni kutoa zawadi hata kama usiku!

No comments: