Tuesday, April 22, 2014

Nimeipenda bustani ya nyumba hii

Kila nikipita barabara hii iliyopo Tandika navutiwa na bustani ya majani inayotunzwa vizuri kando ya nyumba hii. Nyumba hii haiko Masaki iko Tandika lakini bustani yake inavutia. Cha ajabu jirani zake wameshindwa kuiga. Si vibaya kuiga jambo zuri. Swali ninalojiuliza, je viongozi wa mtaa huu hawaioni bustani hii na kuwashawishi wenye nyumba kando ya barabara hii kutengeneza bustani ndogo kama hii. Itapendeza na itavutia. Tuwe wabunifu kwenye makazi yetu. Si dhani kuwa kuitunza bustani hii ni gharama kubwa.

1 comment:

Faustina said...

Unajua watu wengi hawaoni umuhimu wa bustani. Kuna mtu alinikuta napanda nyasi kwa garden yangu akanicheka kwa dharau sana na kaniambia baadala ya kupanda maboga matembele natupa tu nguvu zangu.nikamwambia apande mboga kwake na nitamuungisha kwa kununua hizo mboga.
Nataka kusisitiza watu wengi bustani za maua hawaoni umuhimu wake.