Tuesday, April 8, 2014

Tanzania 'Bingwa wa Kandanda wa Dunia' 2014

Bingwa ni Bingwa tu. Ndiyo, Tanzania tumekuwa Bingwa wa Kandanda wa Dunia  kwa Watoto wa Mitaani mwaka 2014. Ni gazeti  la Daily News pekee lililoipa umuhimu wa kwanza habari hii katika ukurasa wake wa michezo toleo la tarehe 8/4/2014. Hii ni habari kubwa katika michezo. Nashangaa kuona hata magazeti ya michezo hayakutoa kipaumbele kwa habari hii kwenye magazeti yao. Mengi yanaandaika habari za Manchester United, Barcelona, Chelsea, Liverpool!  Zinatuhusu nini Watanzania. Watoto wa Mitaani wametuletea sifa Watanzania. Waliondoka wakiwa na maandalizi hafifu. Hawakukata tamaa. Safari tu kwao ni motisha. Kutoka mtoto wa mitaani hadi kupanda ndege kuna tofauti kubwa sana. Kutoka mitaani hadi kwenda kuishi hoteli zenye hadhi ya Kimataifa ni hadhi kubwa sana. Mimi nimefurahishwa sana na matokeo haya. Kijana pichani  anayepeperusha bendera ya Taifa hata jina halijulikani anaonekana kuwa na furaha ya pekee. Iko siku atakuja kuwa maarufu. Tunasoma kuwa wachezaji wengi kutoka Amerika ya Kusini wametoka kwenye familia duni na kuwa maarufu katika Soka Duniani. Hawa huwa na bidii sana wanapopata kitu cha kushika. Hivi bado hatujafumbuka macho na kuweza kuanza kuwekeza huko mitaani. Kuwa mtoto wa mtaani si dhambi, yote ni maisha. HONGERA TANZANIA KWA KUTWAA UBINGWA WA DUNIA. (Picha kwa hisani ya gazeti la Daily News 8/4/2014)

4 comments:

JUMUIYA YA BIKIRA MARIA MALKIA WA MALAIKA said...

kweli ni muhimu kujipongeza kwa kazi nzuri!

kigunizi said...

Banzi sie machizi fresh hatuyaoni ya kwetu bali hupenda kusifia ya wnzetu ,hawa watoto tangu wanaondoka hawakuripotiwa kama inavyostahili.Hivi sasa wanajaribu kuripoti kwasababu wanaona aibu kwakuwa wamechukuwa kombe .Ingekuwa habari za fitina za Yanga na Simba wangeripoti mapema .

Innocent John Banzi said...

Kigunizi asante kwa maoni yako na pia nashukuru kwa kusoma blog yangu

Innocent John Banzi said...

Bikira Maria, nashukuru kwa kusoma post hii na kutoa maoni.