Tuesday, April 8, 2014

Viongozi katika dua

Ninaamini kuwa kiongozi bora ni yule anayemuamini Mungu na ni mtu wa sala.. Pichani bila kujali nyadhifa zao Viongozi wetu wa Taifa  wakiomba dua wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume  huku wakiwa na vitabu vya sala. Kwa haraka haraka naweza kuwatambua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania -Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dr. Mohamed Shein, Makamu wa Rais Dr. Mohamed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa Awamu ya pili  Mzee Ali Haasan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Amani Abeid Karume, na Makamu wa Pili wa Serikali ya Zanzibar Balozi Seif Iddi Ali (Picha kwa hisani ya Gazeti la Daily News 8/4/2014)

No comments: