Tuesday, February 17, 2009

Mwalimu "nakutiire!"

Hivyo ndivyo alivyoshangaa mwanafunzi kutoka mkoa wa Kagera kwa kuona mwalimu wake akichapwa- Mwalimu "nakutiire."- Mwalimu amechapwa. Nilisikia leo asubuhi kwenye kipindi cha radio moja maarufu hapa jijini. Kweli walimu wetu wamefedheheshwa. Walimu sasa wanachapwa hata na polisi!

Mke wangu ni mwalimu, sijui ingekuwaje kama mke wangu naye angekuwa mmojawao aliyechapwa tena kwa amri ya DC! Tumeshindwa kuwaheshimu walimu hadi kufikia hali hii. Nani atapenda kuwa mwalimu?

1 comment:

Belo said...

Kwa kweli ni udhalilishaji wa hali ya juu,yaani pamoja na walimu kunyanyaswa ikiwa pamoja na kutolipwa fedha zao na mishahara midogo then DC anamchapa bakora eti kisa wanafunzi wamefeli,huyo jamaa anastahili kwenda jela naye akale bakora