Tuesday, February 3, 2009

Tukiwapa motisha askari wetu wa barabarani watadhibiti ajali

Kwa muda wa dakika tano kwa siku ya leo nimeona niandike tena kuhusu ajali kwani ni janga linalostahili kuvaliwa njuga.

Leo asubuhi wakati nikienda kazini nilifurahi kuona magari yakienda kwa mtiririko unaotakiwa kwenye barabara ya Kilwa huwezi kuamini kuwa tulitumia dakika 45 kutoka Kisemvule hadi TAZARA.

Kwanini imekuwa hivyo? Askari wa barabarani na wa FFU ("tigo") walijipanga vyema kwenye sehemu korofi. Kwahiyo hakuna dereva aliyediriki kuchepuka. Matokeo yake usafiri ulikuwa safi na wa salama. Sijui kama askari hawa wamepewa motisha. Lakini naamini kuwa iwapo itapangwa motisha ya aina fulani kwa askari wanaolinda usalama wa barabarani nina uhakika tutapunguza ajali za barabarani na kurahisisha usafiri hapa jijini na kwenye barabaraba zetu za kwenda mikoani.

No comments: