Thursday, February 26, 2009

TUWE NA TABIA YA KUJISOMEA

Watanzania tulio wengi hatuna tabia ya kujisomea. Hata kwa wasomi wakishapata shahada zao mchezo umekwisha. Ukisafiri kwa ndege, bus, treni, meli ni nadra sana kuwakuta watu wanasoma. Ni wachache utawakuta wameshika angalau gazeti! Lakini ni wazuri kwa porojo tena zisizo na uhakika za kusikia tu, za vijiweni tu. Kwanini tusisome vitabu mbalimbali, majarida mbalimbali? Kama wewe mpenda mpira wa miguu basi angalau uwe unajisomea majarida mbalimbali ya soka. Kama wewe ni mfanya biashara kuna majarida mbalimbali hata kwa kiswahili yanayoelezea biashara.Tukisoma tunajiongezea maarifa. Tunaweza kujenga hoja za msingi tunaweza kuweka mikakati mizuri itakayoweza kutusaidia katika kuboresha maisha yetu. Tusome ili watoto wetu wajifunze kutoka kwetu. Tusilalame na kushuka kwa kiwango cha elimu nchini hata sisi watu wazima hatusomi!

No comments: