Monday, February 2, 2009

Tunapenda kula wali lakini........!

Jumamosi na hata siku ya Jumapili (jana) blog hii ilifanya kazi kwenye plot ya mpunga. Kwa shughuli za kupanda na kupandikiza.

Jamani lazima niseme ukweli kilimo cha mpunga ni shughuli pevu. Shughuli ya kupanda na kupandikiza ni shughuli ngumu sana. Sasa ninafahamu kwanini bei ya mchele ni kubwa sana kuliko mahindi. Kustawisha mpunga ni kazi. Nawapongeza wakulima wa mpunga. Nimejifunza kuwa kama kweli Tanzania tumedhamiria kuinua uzalishaji wa mazao ya kilimo inatubidi kuwekeza kwa kiasi cha kutosha kwenye kilimo.

Tuwekeze kwenye zana ili zirahisishe kazi ya shambani, tuwekeze kwenye mbegu bora ili tuweze kuvuna mpunga mwingi na mzuri, tuwekeze kwenye pembejeo nyingine kama vile madawa na mbolea vinginevyo uzalishaji utaendelea kuwa mdogo mwaka hadi mwaka na hivyo kufanya mpunga kuwa mchache sokoni matokeo yake ni kupanda kwa bei ya mchele. Uzalishaji unapokuwa mdogo na mahitaji makubwa ni dhahiri bei itapanda tu.

No comments: