Monday, December 29, 2008

Mto wa Mfizigo na mawe yake

Mto wa mfizigo ni moja ya mito mikubwa katika tarafa ya Matombo. Mto huu humwaga maji yake katika mto wa Ruvu ambapo wakazi wa jiji la Dar Es Salaam pamoja na sehemu za mkoa wa Pwani hapata maji kutoka mto huu.

Pamoja na umuhimu wake wa kutoa maji, mto huu una aina mbalimbali ya mawe ya kuvutia sana. Licha ya kuufahmu mto mfizigo kwa muda mrefu kwani nimeutumia mto huo kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kuoga, kufua, kuvua samaki, kuchota mchanga na mawe tangu nikiwa mtoto sikuweza kutambua hapo awali kuwa mto Mfizigo una mawe ambayo yakipangwa vizuri yanaweza kutoa mapambo ya kuvutia. Ni juzi tu nilipokuwa mtoni Mfizigo ndipo wazo lilinijia la kuokota kiasi cha mawe ya aina mbalimbali ambayo yalinivutia sana. Ajabu, mto Mfizigo, mawe yake yanavutia sana.

1 comment:

mnzeru said...

Bwana Banzi na mimi nimeliona hilo. mwaka wa juzi nilikwenda washington na kujionea wenzetu wanavyotumia mawe hayo kwa tekinolojia ya kisasa kabisa kupamba nyumba zao. sasa usiseme sana wajanja wasije wakatuwahi bwana. Na mimi nimekamata sana ningu, mangala, vinindi na ngadu tangu kwa mpishi mpaka mafufumwe kule juu karibu na konde. kwa hiyo changamka hiyo ni pesa bwana!!!