Wednesday, March 11, 2015

Wadau wa EAAPP wanavyoridhishwa na njia za kupata teknolojia

 'Eastern Africa Agricultural Productivity Project' (EAAPP) ni mradi unaolenga kuongeza uzalishaji na Tija kwenye Kilimo kwa nchi za Mashariki ya Afrika. Maradi huu unatekelezwa katika nchi 4 nazo ni Tanzania (Mpunga);Kenya(Ng'ombe wa Maziwa;Uganda (Muhogo) na Ethiopia(Ngano). Mazao yaliyo kwenye mabano yanaonyesha zao kuu linaloshughulikiwa katika nchi hiyo ambapo vituo mahiri vya mazao hayo vinaimarishwa (Regional Centres Of Excellence). Hapa Tanzania, kituo mahiri cha zao la mpunga kiko katika kituo cha Utafiti wa Kilimo-KATRIN, Ifakara. Moja ya viashiria vya mradi huu ni kupima kiwango cha wadau kuridhika na upelekekaji wa teknolojia za kilimo kwa kutumia njia tofauti kama vile radio,TV, vipeperushi,mafunzo na maonyesho ya kilimo. Kwa kuzingatia chart hiyo hapo juu, inaonyesha kuwa wadau hadi kufikia mwaka huu (2015) wadau wameridhika kwa asilimia 67 ukilinganisha na asilimia 20 iliyokuwepo mwaka 2010.Haya ni mafanikio makubwa.

No comments: