Monday, June 8, 2009

Makutupora nyumbani kwa zabibu


Kituo cha Utafiti wa Kilimo Makutupora ndicho kituo pekee kinachofanya utafiti wa zao la zabibu hapa nchini. Kituo hiki kipo mkoani Dodoma. Mkoa wa Dodoma pia ni maarufu kwa kilimo cha zabibu ambalo ni zao muhimu la biashara kwa wakulima wa Dodoma. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Utafiti Kanda ya Kati Mtafiti Leon Mrosso, utafiti wa zao hilo umekiwa ukifanyika kituoni hapo kwa takribani miaka 30 sasa na kupata mafanikio makubwa yakiwemo uzalishaji wa aina bora za zabibu . Kwa mfano mwaka 2007 kituo kimeweza kutoa aina mbili za zabibu -Makutupora red na Chenin white ambazo zote ni za kutengeneza mvinyo. Kituo pia kinatafiti aina ya zabibu za kutafuna kama vile Makutupora white,Black Rose, na Regina. Pichani shamba la majaribio la zabibu kituoni Makutupora.

No comments: