|
Shule ya msingi Lanzi |
Banzi wa Moro ni mzaliwa wa Morogoro vijijini, tarafa ya Matombo. Jana nilipata nafasi ya kutathmini matokeo ya Darasa la saba kwa mwaka 2013 kwa wilaya ya Morogoro vijijini kwa shule chache ninazozifahamu kama vile Matombo, Konde, Kitungwa, Gozo, Kibungo,Kibangile, Tununguo, Nyachiro,Lanzi,Kungwe. Wastani wa ufaulu kwa shule hizi ni D. Nina maswali mengi yasiyo na majibu. Je, shule hazina walimu? Mazingira si mazuri, hakuna ushirikiana kati walimu na wazazi? Wangapi wameiona hali hii. Wangapi wanakerwa na matokeo haya? Kwetu sisi Moro matokeo haya si mazuri. Shule iliyojitahidi ni ya 3044 kitaifa nayo ni Kibangile. Shule za siku nyingi kama vile Matombo ni ya 10705 kitaifa? Hivi Matombo ina shida gani? Wazawa kutoka Morogoro tuyafanyie kazi matokeo haya na tuje na mapendekezo. Kwa mfano picha ya hapo juu inaonyesha darasa mojawapo ya shule ya msingi Lanzi. Sijui kama kuna mabadiliko (Picha kutoka mitandaoni)
No comments:
Post a Comment