- Yeye ni binadamu na hivyo ipo siku atakufa tu na kuachia madaraka. Kama ana hofu kwamba hakuna Mtanzania mwingine anayeweza kushika urais, je akifa itakuaje?
- Mwalimu alisema kama yeye asingeachia madaraka, hakuna kiongozi mwingine wa Tanzania ambaye angekubali kuachia madaraka. Hivyo alitaka kutengeneza mfumo au utaratibu wa kupokezana vijiti. "Kwa maelezo yake mwenyewe Mwalimu alisema kama tutaweza kupokezana madaraka kwa muda wa miaka 30 hadi 40 mfululizo, huo utakuwa utaratibu wa kudumu na hakuna atakayeupindua.
- Tatu, Mwalimu alisema alitaka kuangalia mwenyewe na kusaidia pale inapowezekana kwenye masuala ya kitaifa. Kuhakikisha Katiba inafuatwa, Awe nje lakini afuatilie kile kinachoendelea na kuona kwamba mpokezano huu wa madaraka unaendelea.
Wednesday, November 13, 2013
Sababu tatu za Mwl.Nyerere kung'atuka
Balozi Charles Sanga aliyefanya kazi na Mwalimu kama Msaidizi wake maalumu katika miaka yake saba ya mwisho hapa duniani,katika mahojiano yake na gazeti la Rai Mwema, ameweka wazi sababu tautu kuuu zilizomfanya Mwl. Julius Kambarage Nyerere (Baba wa Taifa) kung'atuka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment