Tuesday, February 3, 2015

Fursa ya kuongea na wafugaji

Tulipopata nafasi ya kuongea na mfugaji Longido Shambakubwa wa Dakawa, Morogoro (mwenye suti) alionekana kujiamini na kuwa na uelewa mpana kuhusu ufugaji na kuwa na mipango endelevu. Kwa maneno yake mwenyewe, ujasiri huu ameupata kupitia mafunzo ya ufugaji wa ng'ombe wa maziwa  pamoja na ziara za mafunzo ndani na nje ya nchi(Nairobi, Kenya) yaliyoandaliwa na Mradi wa EAAPP. Wakulima wakipata mafunzo pamoja na kuwatembelea wakulima wenzao  wanabadilika haraka katika upokeaji wa teknolojia za kisasa za kilimo na ufugaji.

No comments: