Wednesday, July 9, 2008

Matunda ya Kutengeneza Amarula yanapatikana Tabora

Kile kinywaji maarufu cha Amarula kinachotengenezwa Afrika ya Kusini na kupendwa sana na wanawake hapa Tanzania, matunda yake yanapatikana kwa wingi kwenye misitu ya Miombo huko Tabora. Watafiti wa kituo cha Utafiti wa Kilimo Tumbi, Tabora wamegundua. Matunda hayo yapo kwa wingi ingawa yanapatikana msituni.

Iwapo utafiti wa kina utafanyika, miti hiyo inaweza kuoteshwa na kuzalishwa kwa wingi hivyo kutoa matunda ya kutosha na kuwezesha wakulima kujiongezea kipato kwa kuuza matunda hayo ya Amarula.

2 comments:

Hector Mongi said...

Nashukuru kwa habari hii. Ni kweli kuwa huenda kituo cha Utafiti Tumbi kikawa chanzo cha taarifa mbalimbali zihusuyo mmea huuu wa Amarula hapa Tanzania na kwingineko kusini mwa Afrika.

Innocent John Banzi said...

Asante Mongi kwa kunisoma. Kazi njema. Je umeshamaliza kabisa kitabu?