Thursday, February 11, 2010

MBARAKA MWINSHEHE MWARUKA



Leo kwenye blog ya Maggid nimepata kusoma habari fupi ya marehemu Mbaraka Mwishehe Mwaruka gwiji la muziki miaka ya sitini aliyebobea mjini Morogoro.

Mbaraka kwa kweli asili yake ni Mzaramo lakini wengi hudhani kuwa ni Mluguru. Huyu aliweza kutunga na kuimba nyimbo nyingi za Kiluguru zikiwemo:- Kukala hamwe ng'avhinogile nibita kuja Mwembosongo, pinga yumwe kanikema kanilongela nibete........ (Kukaa mahali pamoja panachosha kwahiyo katika pitapita zake kule Mwembesongo binti mmoja akamwambia nisubiri.....); Mnzese gwe mnzese kolima (Anamwimba ndege mmoja anayeitwa Mnzese mjanja sana kwa kuimba lakini hana anachokifanya shambani....); Jamani Morogoro, Morogoro, oh oo, maji yatiririka vilimani oh oh na hiyo aliyoining'iniza MJENGWA kwenye blog yake . Wajomba wamechacha wamekuja juu harusini.........

Kwa kweli Marehemu Mbaraka Mwinshehe alitunga nyimbo zenye kugusa jamii. Hakuimba mapenzi pekee. Lala salama Mbaraka falsafa yako bado inadumu kizazi hadi kizazi. (Picha kwa hisani ya Blog ya MJENGWA).

2 comments:

HOOVER said...

I created a Mbaraka Mwinshehe Facebook page. Nitaweka link ya hii post yako pamoja na hiyo ya Maggidi.

Captain said...

Ama kweli Africa ya mashariki haijawahi pata muimbaji/mtunzi kama marehemu Mbaraka. Lala salama