Monday, January 26, 2009

Wavivu wa kuweka kumbukumbu

Nimegundua tatizo la watu wengi hasa sisi Watanzania hatupendi kuweka kumbukumbu ya shughuli zetu. Awe msomi, mkulima, mfanya biashara, mwalimu, fundi....................
Hatuweki kumbukumbu na hii ni hatari. Hatuwezi kujua gharama tulizotumia. Vitu tulivyokuwa navyo, wadeni wetu...........

Kwa hali hiyo basi hatuwezi kuwa na mipango sahihi kwa sababu hatuna data! Blog hii imekuwa ikijishughulisha na kilimo cha mpunga huko Kisemvule tangu mwezi Desemba. Imelipa vibarua wa kufyeka, kukatua, na kununua mbegu. Tayari sehemu fulani mpunga umeshapandwa lakini tarehe ya kupanda mpunga huo haifahamiki. Kweli ni wavivu wa kutunza kumbukumbu na hii ni hatari kwa maendeleo yetu.

1 comment:

Belo said...

Ni kweli kabisa wengi tunashindwa kuweka malengo yetu kila mwaka na hata tukiweka hatuyazingatii
Ni vizuri kuweka kumbukumbu ya tuliyo fanya ili baadae tufanye utafiti kama tumefanikiwa au la ili tuongeze bidii au kubadilisha mbinu