Thursday, July 22, 2010

Damu ya Kristu Nancy


Mwaka 1997 tarehe 2/8/1997 nilifunga pingu za maisha na mke wangu mpenzi Nancy Ireneus Mbawala katika Kanisa Katoliki Mashahidi wa Uganda-Magomeni jijini Dar Es Salaam kwa hiyo ifikapo tarehe 2/8/2010 tutatimiza miaka 13 ya ndoa. Tumejitahidi siyo. Pichani Nancy akinywa damu ya Kristu siku ya harusi yetu.

4 comments:

sophia kizito said...

Hongera Banzi kwa kutimiza miaka 13 ya ndoa, kufika hapo sio mchezo, wengine wanafika miezi wakijitahidi sana mwaka! naomba umpende sana Nancy kama ulivyokuwa ukimpenda siku hii, ikiwezekana kila siku iwe siku ya harusi. jitahidi to maintain hiyo hali,hadi kifo kiwatenganishe.

Innocent John Banzi said...

Shem Sophia, Asante sana kwa ushauri wako mzuri. Maisha ya ndoa yanahitaji upendo, uvumilivu na zaidi kutunza siri za ndani. Nashukuru kwa kupitia blog hii ya Banzi wa Moro natumaini utakuwa utaitangaza kwa wengine ili kupitia blog hii tuweze kuwasiliana na kushauriana kwa maendeleo ya familia zetu pamoja na Taifa.

Belo said...

Hongera, nakutakia baraka kwenye ndoa yenu pamoja na kina Maria,Cathy na Sist

Innocent John Banzi said...

Ndiyo Belo.Ndoa inahitaji maamuzi ya dhati kati yenu wawili. Aidha ndoa inahitaji kujiimarisha kila wakati. Inawezekana matazamio hayakuwa hivyo ni vyema kujiuliza kwanini kuna mabadiliko na inapotokea kuna matatizo ni vyema kuyapatia ufumbuzi wa haraka kabla hayajafika kwa wengine.