Friday, July 30, 2010

Hii ndiyo timu ya wapelembaji


Idara ya utafiti na Maendeleo iliyoko Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika imeweka utaratibu mzuri wa kupelemba na kutathmini shughuli za utafiti katika kanda zake saba za utafiti ili kuweza kufahamu utekelezaji wa mipango ya utafiti ufanisi, changamoto na kuweka mikakati ya kupambana na changamoto zinazojitokeza. Pichani wanaonekana wapelembaji waliotumwa kanda ya kaskazini mwezi Juni 2010.

3 comments:

Belo said...

Naomba kuuliza maana ya Kupelemba

Innocent John Banzi said...

Belo maana ya kupelemba ni kudadisi kwa kutumia nyenzo mbalimbali ili uweze kupata taarifa unazozihitaji kwa kuzingatia viashiria (indicators) vilivyowekwa. Kwa kiingereza wanaita Monitoring.

Belo said...

Asante ,kweli Watanzania hatujui Kiswahili