Tuesday, July 23, 2013

Wameamua kulima bustani ya mboga kijijini Kisemvule

Bw. Peter  Linus Mkude (Mwenye shati jekundu) na rafiki zake wawili (mmojawapo mwenye shati jeupe) wameaumua kulima bustani ya mboga mboga. Kwa kuanza tayari wameshaandaa eneo lipatalo nusu eka na kupanda matikiti maji. Ni wazo walilokuja nalo kujikwamua kiuchumi. Tarehe 21/7/2013 nilipata kutembelea sehemu hiyo iliyopo kijijini Kisemvule wilaya ya Mkuranga mwanangu Maria pichani kushoto na rafiki yake nao walikuwa na shauku ya kuona shamba hilo.

No comments: